Mamlaka nchini niger imetangaza amri ya kutotoka nje katika eneo lenye hali tete la tillaberi

Majaribio mengine mawili ya kutoroka gereza hilo ya mnamo 2016 na 2019 yalizimwa na maafisa wa usalama

Mamlaka nchini Niger imetangaza amri ya kutotoka nje katika eneo lenye hali tete la Tillaberi baada ya wafungwa kadhaa kutoroka katika gereza yenye ngome nyingi inayojulikana kuwa na idadi kubwa ya wanajihadi.


Tukio hilo lilitokea siku ya Alhamisi katika gereza la Koutoukale lililoko takriban kilomita 50 kaskazini-magharibi mwa mji mkuu, Niamey, wizara ya mambo ya ndani ilisema.

Majaribio mengine mawili ya kutoroka gereza hilo ya mnamo 2016 na 2019 yalizimwa na maafisa wa usalama.

Vikosi vya kijeshi vya Niger vimelemewa na mashambulizi ya wapianaji wa jihadi magharibi na kuwalinda utawala wa kijeshi ambao ulichukua mamlaka kwa mapinduzi ya mwaka jana.

Share: