Mama karume awasili arusha kwaajili ya halfa ya kumbukizi ya sokoine

Mke wa Rais wa kwanza wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Abeid Karume, Fatma Karume (95) amesema anafurahishwa na utendaji wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan na kuahidi kumpigia kampeni katika uchaguzi mkuu ujao.

Mama Fatma Karume ametoa kauli hiyo na kusema kwamba Rais Samia ni matokeo ya mapambano ya muda mrefu ya kupambana kuwaweka wanawake katika nafasi za juu za maamuzi na kumtaja kama Kielelezo Sahihi cha kuonesha umadhubuti wa wanawake viongozi.

Mama Fatma ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mh. Paul Makonda mara baada ya kuwasili mkoani Arusha ili kuhudhuria Misa maalumu ya miaka 40 tangu kifo cha Hayati Edward Moringe Sokoine, aliyekuwa Waziri mkuu wa Tanzania.

Kwa Upande wake mkuu wa Mkoa Mh. Makonda amemueleza Mama Fatma kuwa Rais Samia Amemuelekeza kushughulika na changamoto mbalimbali za wananchi na kueleza namna ambavyo Rais Samia ameweka fedha nyingi mkoani hapa katika kusisimua Utalii wa Arusha na utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

Hayati Sokoine alikuwa Waziri mkuu wa Tanzania na alifariki Aprili 12, 1984 kwa ajali ya gari. Ijumaa Aprili 12,2024, Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwaongoza watanzania kwenye Misa maalum ya miaka 40 ya kumbukizi ya kifo cha Sokoine.





Share: