Mama janet magufuli amtaka rc makonda kuwatetea wananchi

Hayati Sokoine alikuwa Waziri Mkuu wa tatu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mama Janet Magufuli, Mke wa aliyekuwa Rais wa awamu ya tano nchini Tanzania amemtaka Mkuu wa mkoa wa Arusha Mh. Paul Makonda kuendelea kuwatetea wananchi na kushughulika na kero zao.

Mama Janet ametoa kauli hiyo mbele ya Mh. Makonda mara baada ya kuwasili jijini Arusha kuhudhuria Misa maalumu ya kumbukumbu ya miaka 40 ya kifo cha aliyekuwa Waziri wa Tanzania Hayati Edward Moringe Sokoine itakayofanyika kesho Ijumaa huko wilayani Monduli mkoani Arusha.

Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Arusha Mh. Makonda ameahidi kuendelea kujitoa katika kuwatumikia wananchi wa Arusha na kumshukuru Mama Janet kwa kumuombea kheri katika kazi zake.

Hayati Sokoine alikuwa Waziri Mkuu wa tatu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Aliwahi kuwa Waziri Mkuu mara mbili, tangu tarehe 13 Februari, 1977 hadi 7 Novemba, 1980 na mara ya pili kuanzia tarehe 24 Februari, 1983 hadi tarehe 12 Aprili, 1984 alipofariki kwa ajali ya gari.




Share: