Uamuzi huo wa kesi umeripotiwa kuibua maswali kwa Wananchi wanaohoji jinsi Serikali inavyoshughulikia mashtaka ya Rushwa na Ufisadi
Mkurugenzi wa Mashtaka wa Serikali (DPP) amefuta Kesi ya Madai ya kupokea Rushwa iliyokuwa inamkabili Makamu wa Rais, Dkt. Saulos Chilima baada ya upande wa Serikali kuwasilisha notisi ya kusitisha kesi hiyo
Dkt. Chilima alikamatwa Novemba 2022 na kushtakiwa kwa tuhuma za kupokea Rushwa ili kutoa Zabuni za Serikali kwa Xaviar Ltd na Malachitte FZE, kampuni zinazohusishwa na Mfanyabiashara wa Uingereza, Zuneth Sattar ingawa pande zote zilikanusha tuhuma hizo
Uamuzi huo wa kesi umeripotiwa kuibua maswali kwa Wananchi wanaohoji jinsi Serikali inavyoshughulikia mashtaka ya Rushwa na Ufisadi hasa yanaowagusa Viongozi. Kwa mujibu wa Katiba, DPP atakuwa na siku 10 kulieleza Bunge sababu za Serikali kuondoa kesi hiyo