Malalamishi yaibuka kuhusu oparesheni ya kikatili ya kijeshi nchini ghana

Wabunge nchini Ghana wanadai uchunguzi ufanyike juu ya madai ya ukatili wa kijeshi dhidi ya vijana wa Garu kaskazini-mashariki mwa Ghana na wahusika kufikishwa mahakamani.

Wabunge nchini Ghana wanadai uchunguzi ufanyike juu ya madai ya ukatili wa kijeshi dhidi ya vijana wa Garu kaskazini-mashariki mwa Ghana na wahusika kufikishwa mahakamani.

Wanajeshi wanadaiwa kuvamia jamii siku ya Jumapili katika kile kinachoonekana kuwa ni shambulio la kulipiza kisasi kufuatia shambulio dhidi ya maafisa wa ujasusi wa usalama wa taifa waliotumwa huko kupambana na ugaidi.

Wabunge wa maeneo bunge ya Garu na Tempane, ambao wanashinikiza uchunguzi huo ufanyike, wamelaani mashambulizi hayo na wanatoa wito wa kuondolewa mara moja kwa wanajeshi katika eneo hilo.

Wabunge hao pia wanataka vijana waliokamatwa waachiwe huru na waliojeruhiwa katika mchakato huo walipwe fidia na serikali.

Picha zilizosambazwa sana kwenye mitandao ya kijamii zilionyesha baadhi ya vijana wakiwa na majeraha mbalimbali, yakiwemo majeraha kwenye miili yao na nyuso zilizovimba.Wale waliojeruhiwa kwa sasa wanapokea matibabu katika Hospitali ya Wilaya ya Garu, ambayo ripoti za vyombo vya habari zinaonyesha kuwa imejaa watu waliojeruhiwa.

Baadhi ya vijana hao pia wanasemekana kutoroka eneo hilo kwa kuhofia kukamatwa na kunyanyaswa na wanajeshi.

Baadhi ya watumiaji wa mitandao ya kijamii wamelaani operesheni hiyo ya kikatili ya usalama.

Hata hivyo, Wizara ya Usalama wa Taifa ya Ghana imekanusha madai hayo, ikisema operesheni ya usalama ilianzishwa ili kunasa silaha zilizotumiwa na kundi la magenge kuwashambulia maafisa wake wiki iliyopita

Share: