Makamu wa Rais wa Marekani Kamala Harris anatarajiwa kumtangaza mgombea mwenza wake kesho Jumanne. Kwa mujibu wa vyanzo vya ndani vya taarifa hiyo, vimeeleza kuwa Kamala amewahoji wagombea kadhaa wa nafasi hiyo katika makaazi yake mjini Washington mwishoni mwa wiki.
Maswali yamekuwa mengi kuhusu uamuzi wa ni nani atakayemteua kuwa mgombea mwenza? yatajibiwa kesho mjini Philadelphia, kabla ya wawili hao kuelekeza kampeni zao katika majimbo yenye ushindani mkali. Wagombea wakuu watatu waliohojiwa katika nafasi hiyo ni gavana wa Minnesota, Tim Walz, Seneta wa Arizona, Mark Kelly, na gavana wa Pennsylvania, Josh Shapiro.
Share: