Makamu wa rais dkt. mpango amewasili mkoani arusha ikiwa ni maandalizi ya maadhimisho ya miaka 40 tangu alipofariki hayati sokoine

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Isdor Mpango amewasili mkoani Arusha leo Alhamisi, Aprili 11, 2024 kuhudhuria maadhimisho ya miaka 40 tangu kilipotokea kifo cha aliyekuwa Waziri Mkuu wa Tanzania Hayati Edward Moringe Sokoine.

Makamu wa Rais Dkt. Mpango amepokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mheshimiwa Paul Christian Makonda akiambatana na viongozi wengine wa serikali ya mkoa wa Arusha.

Kulingana na taarifa ya Mkuu wa mkoa, maandalizi ya maadhimisho hayo yatakayofanyika kijiji cha Enguiki, wilayani Monduli yamekamilika kwa asilimia kubwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye kumbukizi hiyo ya miaka 40 tangu alipofariki Hayati Sokoine.

Share: