Majaliwa: tunaendelea kufikisha umeme kwenye vitongoji

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na Wakazi wa Issenyi, Wilaya ya Serengeti mkoani Mara ambapo alisema Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) inaendelea na kazi ya kupeleka umeme kwenye vijiji ambapo kazi kubwa imefanyika na sasa nguvu kubwa inaelekezwa kwenye kufikisha umeme kwenye vitongoji.

Pia Mheshimiwa Majaliwa ametoa rai kwa Watanzania kuachana na matumizi ya kuni na mkaa badala yake waanze kutumia gesi.

Aidha alisema kuwa kutokana na uwekezaji mkubwa uliofanywa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye sekta ya elimu, hakuna sababu ya mzazi kutompeleka mtoto shule “Tumepiga marufuku michango ya hovyo hovyo ambayo ilikuwa ni kero kubwa kwa wazazi,pia tumeimarisha miundombinu ya kutolea elimu”

Share: