MAHAKANI NCHINI KENYA YA AMURU MWANGI AKAMATWE

Yamkuta mazito mwanaharakati maharufu nchini Kenya Mwangi,baada ya kustakiwa na kutakiwa kufika mahakamani ,Boniface Mwangi ni mpiga picha, mwanaharakati, na mjasiriamali wa kijamii kutoka Kenya, anayejulikana kwa juhudi zake za kupigania haki za binadamu, kupinga ufisadi, na kuhamasisha mabadiliko ya kisiasa kupitia sanaa na maandamano. Alizaliwa tarehe 10 Julai 1983 huko Taveta, mkoani Taita-Taveta, Kenya .

Mahakama moja nchini Kenya imetoa hati ya kukamatwa kwa mwanaharakati maarufu Boniface Mwangi, baada ya kushindwa kufika mahakamani kujibu mashtaka ya kumshambulia afisa wa polisi.


Kwa mujibu wa waraka wa mashtaka, Mwangi alitakiwa kufika mahakamani lakini alikosa kufanya hivyo, jambo lililopelekea mahakama kutoa agizo la kukamatwa kwake. Kesi hiyo sasa imepangwa kusikilizwa tena Julai 14, 2025, mbele ya Mahakama Nambari 1.


Hapo awali, mwanaharakati huyo alidaiwa kujaribu kuingia nchini Tanzania kinyume na taratibu, akidaiwa kufuatilia kwa karibu kesi inayomkabili Kiongozi wa Upinzani kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Share: