Madereva wa treni wagoma ujerumani

Ratiba ya dharura ya safari za treni inatumika huku asilimia 80 ya huduma za kawaida za masafa marefu zikifutwa kabisa.

Mgomo wa madereva wa treni wa Ujerumani umesababisha huduma za usafiri wa abiria kote nchini kukaribia kukwama kabisa mapema leo asubuhi.

Shirika la usafiri wa treni Ujerumani, Deutsche Bahn limetangaza kwamba madereva wengi walianza mgomo wao mwendo wa saa nane usiku wa manane.

Mgomo wa treni za mizigo ulianza siku ya Jumanne saa kumi na mbili jioni. Mgomo huo utaendelea hadi Ijumaa jioni saa kumi na mbili jioni.

Ratiba ya dharura ya safari za treni inatumika huku asilimia 80 ya huduma za kawaida za masafa marefu zikifutwa kabisa.

Deutsche Bahn imesema kutakuwa pia na athari kwa huduma za treni za masafa mafupi, ingawa upana wa athari zake utatofautiana kutoka eneo moja hadi lingine.

Share: