Alimpokea Bassirou Faye, ambaye alikuwepo na mfadhili wake Ousmane Sonko, katika ikulu ya rais mjini Dakar siku ya Alhamisi.
Rais wa Senegal, anayemaliza muda wake, Macky Sall, amekutana na mrithi wake Bassirou Diomaye Faye kwa mara ya kwanza tangu Faye ashinde uchaguzi wa rais uliofanyika Jumapili, na kumshinda mgombea wa muungano tawala Amadou Ba.
Alimpokea Bassirou Faye, ambaye alikuwepo na mfadhili wake Ousmane Sonko, katika ikulu ya rais mjini Dakar siku ya Alhamisi.
Maelezo ya majadiliano yao hayakuwekwa wazi. Macky Sall amempongeza rais mteule kwa ushindi wake.
Anatarajiwa kukabidhi madaraka kwa Faye mwenye umri wa miaka 44 mnamo Aprili 2 baada ya kutumikia miaka 12 kama kiongozi wa Senegal.
Share: