Kampuni hiyo inatuhumiwa kughushi vyeti rasmi vya usalama kupitia watengenezaji wakubwa wa magari nchini humo.
Makao Makuu ya Kampuni ya Toyota Motor nchini Japani, yametembelewa na maafisa wa Wizara ya uchukuzi ikiwa ni sehemu ya uchunguzi wa kashfa ya kiusalama.
Kampuni hiyo inatuhumiwa kughushi vyeti rasmi vya usalama kupitia watengenezaji wakubwa wa magari nchini humo.
Masaa machache baada ya Mwenyekiti wa Toyota kuomba radhi kwa udanganyifu juu ya vipimo vya kiusalama katika aina 7 za magari, maafisa hao walifika kwenye Makao Makuu ya Kampuni hiyo.
Baadhi ya vipimo vilivyoghushiwa ni pamoja na vipimo vya nguvu ya injini, vipimo vya mgongano na uharibifu wa kiti cha nyuma wakati wa ajali.
Kufuatia uchunguzi huo, utengenezwaji wa magari aina ya Corolla Fielder, Corolla Axio na Yaris Cross umesimamishwa.