Maafisa wa usalama nchini kenya wamefunga barabara kadhaa muhimu zinazoelekea kwenye majengo ya bunge

Maafisa wa usalama nchini Kenya wamefunga barabara kadhaa muhimu zinazoelekea kwenye majengo ya Bunge kabla ya maandamano makubwa ya kupinga mswada wa fedha.

Barabara za Parliament Road na City Hall Way, miongoni mwa zingine, zimefungwa kwa magari na watembea kwa miguu huku hatua za usalama zikiimarishwa.

Magari ya polisi ya kuzima ghasia na lori zimetumiwa kama vizuizi katika njia kuu zinazoelekea bungeni.

Ufikiaji wa eneo hilo umezuiliwa huku wazi na wafanyikazi walioidhinishwa pekee wakiruhusiwa kufika kwa viitambulisho maalum.

Maandamano hayo, yaliyoandaliwa na mashirika mbalimbali ya kiraia yamevutia uungwaji mkono mkubwa kutoka kwa vijana kote nchini.

Kikosi cha maafisa wa polisi wa kupambana na ghasia kutoka vitengo tofauti pia wametumwa kulinda eneo hilo.

Huku hatima ya muswada wa sheria ya fedha ukining’inia, macho yote yanaelekezwa Bungeni huku wabunge wakijiandaa kuujadili.

Muswada huo unajumuisha marekebisho ya ushuru na matumizi ya umma.

Share: