Maafisa wa israel wamtaka guterres ajiuzulu

Maafisa wa ngazi ya juu wa Israel wamemtaka Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ajiuzulu

Maafisa wa ngazi ya juu wa Israel wamemtaka Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ajiuzulu, kufuatia kauli yake kwamba mashambulizi ya kigaidi yaliyofanywa na Hamas “hayakutokea kwenye ombwe”.

Balozi wa Israel katika Umoja wa Mataifa Gilad Erdan alisema kuna hajya ya katibu Mkuu Antonio Guterresajiuzulu kutokana na matamshi aliyoyataja kuwa yamehalalisha ukatili wa kutisha dhidi ya watu wa Israel.

Aliongeza kwamba Umoja wa Mataifa upo kwa ajili ya kuingilia kati matendo aliyoyainisha ya kikatili kama yanayoshuhudiwa hivi sasa katika mzozo kati ya Israel na Hamas, hivyo kumsisitiza aombe radhi.

Share: