Louisiana jimbo la kwanza la marekani kuweka kila darasa la shule ya umma hadi ngazi ya chuo kikuu bango la amri kumi za mungu

Louisiana imekuwa jimbo la kwanza la Marekani kuagiza kwamba kila darasa la shule ya umma hadi ngazi ya chuo kikuu lazima lionyeshe bango la Amri Kumi [za Mungu]

Hatua hiyo inayoungwa mkono na chama cha Republican iliyotiwa saini kuwa sheria na Gavana Jeff Landry Jumatano inaelezea amri hizo kama "hati ya msingi ya serikali yetu ya jimbo na kitaifa".


Sheria hiyo inatarajiwa kupingwa na mashirika ya kutetea haki za kiraia, ambayo yanadai kuwa inakiuka mgawanyiko kati ya kanisa na serikali unaoainishwa katika marekebisho ya kwanza ya Katiba ya Marekani, yanayojulikana kama Establishment Clause [Kifungu cha Kuanzishwa].

Inasema: "Kongamano halitaweka sheria yoyote kuhusu uanzishwaji wa dini, au kukataza matumizi yake huru."

Sheria ya serikali inahitaji bango lijumuishe maandishi matakatifu katika "herufi kubwa, zinaooweza kusomeka kwa urahisi kwenye bango ambalo ni inchi 11 kwa inchi 14 (sm28 kwa sm35.5) na kwamba amri ndizo "zinapaswa kuonekana vyema " katika tangazo.

Bango hilo linaoneshwa pamoja na "taarifa ya muktadha" ya aya nne ambazo zitaelezea jinsi amri "ni sehemu maarufu ya elimu ya umma ya Marekani kwa karibu karne tatu".

Mabango ni lazima yawekwe katika madarasa yote yanayopokea ufadhili wa serikali kufikia 2025 - lakini hakuna ufadhili wa serikali unaotolewa kulipia mabango yenyewe.

Share: