Lotfi mraihi: mgombea wa uchaguzi ujao wa urais nchini tunisia amekamatwa kwa tuhuma za utakatishaji fedha

Mawakala wa Idara ndogo ya Masuala ya Jinai katika Mahakama ya El Gorgeni, wamemkamata Lotfi Mraihi, Rais wa chama cha Republican na mgombea wa Uchaguzi ujao wa Urais, kwa tuhuma za utakatishaji fedha.

Kwa mujibu wa kituo kimoja cha Redio cha Tunisia, taarifa kutoka kwa Msemaji wa Mahakama ya mwanzo ya Tunis, Mohamed Zitouna, amesema “Rais wa UPR anakamatwa kwa tuhuma za utakatishaji fedha, kuhamisha mali na kufungua akaunti nje ya nchi bila idhini.

Mraihi alikamatwa katika mkoa wa Nabeul (kaskazini-mashariki) na kupelekwa katika Makao Makuu ya Polisi huko El-Gorgeni.

Aprili iliyopita, Maraihi alitangaza, katika video iliyowekwa kwenye ukurasa wake rasmi wa Facebook, nia yake ya kugombea katika Uchaguzi ujao wa Urais Tunisia.

Share: