
Lil Wayne akili kutokuwa na kinyongo na Kendrick Lamar kutumbuiza kwenye super Bowl
Lil Wayne amethibitisha kuwa ameongea na Kendrick Lamar baada ya drama kuhusu shoo ya mapumziko ya Super Bowl ya mwaka 2025, ambapo Kendrick alitangazwa kama mtumbuizaji mkuu. Lil Wayne, ambaye mwanzo alionyesha kusikitishwa na kuachwa kwake, alisema hana kinyongo na amemtakia Kendrick kila la kheri.
Kendrick alizungumzia suala hilo kwenye wimbo wake “wacced out murals” kutoka kwenye albamu yake 'GNX', akisema bidii yake katika kazi ilimvunja moyo Lil Wayne. Lil Wayne alikiri hajawahi kusikia wimbo huo hadi aliposomewa mistari hiyo wakati wa mahojiano, na akaeleza kuwa hakuumia binafsi bali alisikitishwa kwa kupoteza nafasi ya kutumbuiza kwenye mji wa nyumbani kwao.
Lil Wayne alikanusha uvumi kwamba aliandaa wimbo wa kujibu baada ya Kendrick kupuuza simu yake, na akasisitiza kuwa hana mpango wa kutumbuiza Super Bowl kama mgeni maalum kwani hata hatakuwa Marekani wakati huo.