
Rapper kutoka Chicago Lildurk amekana hatia katika kesi yake ya kuhusika kwenye mauaji kwa kupanga njama ya kuua-kwa-kukodi katika mahakama huko Los Angeles baada ya kesi yake kuhamishwa kutoka Miami.
Durk alifikishwa kortini Alhamisi ya jana (Novemba 14), wiki tatu baada ya kukamatwa bila dhamana huko Florida, akidaiwa kujaribu kutoroka na sasa atasalia katika Kituo cha wafungwa cha Metropolitan huko Los Angeles.
Kesi ya kusikilizwa kizuizini imepangwa Desemba 12 ili kubaini kama atapewa dhamana - ama laa.
Share: