Liberia: yoyote aliyehusika na rushwa katika serikali zilizopita na serikali ya sasa kuanza uchunguzi

Rais Joseph Boakai ametangaza kuunda Kikosi Kazi kitakachokuwa na jukumu la Kukabiliana na Vitendo vya Rushwa pamoja na kurejesha Mali za Serikali zilizoibwa kifisadi. 

Rais Boakai ameagiza Kikosi hicho kumtafuta Afisa wa ngazi yoyote aliyehusika na Rushwa katika Serikali zilizopita na Serikali ya sasa pamoja na kuanza uchunguzi dhidi ya tuhuma zitakazobainika. 

Aidha, Rais amesema Mali zote za Serikali zilizouzwa na kununuliwa kinyume na utaratibu zirejeshwe haraka. Uamuzi huo unakuja ikiwa ni Siku 44 tangu aingie Madarakani. 

Share: