Liberia: rais joseph boakai ashindwa kumaliza hotuba baada ya kuapishwa

Rais Joseph Boakai, (79) alishindwa kumaliza hotuba yake baada ya Uapisho ambapo aliongea kwa dakika 30 na kupata changamoto iliyomlazimu kupewa msaada kuondoka kwenye jukwaa wakati wa sherehe ya kuapishwa kwake

Rais Boakai alishindwa mara mbili kuendelea na hotuba yake, na sherehe ikasitishwa. Baadhi ya ripoti zimedai kwamba alipatwa na uchovu wa joto kwani joto lilifikia zaidi ya Nyuzi joto 30

Joseph Boakai ambaye anakuwa Rais mwenye Umri Mkubwa zaidi Liberia, suala la wasiwasi wa Afya yake liliibuliwa mara nyingi wakati wa kampeni ambapo alinukuliwa akisema afya yake ilikuwa nzuri na "umri unapaswa kuwa baraka kwa nchi hii"

Share: