Laac yawakalia kooni watumishi  wasiokuwa na sifa

Kutokana na ubadhilifu wa fedha uliobainika katika mradi wa shule ya sekondari Tura Ofisi ya Rais TAMISEMI ichukuwe hatua stahiki kwa watendaji wote

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) Halima Mdee ametoa maagizo kwa Ofisi ya Rais TAMISEMI kuhakikisha wanapeleka wataalamu waliokidhi viwango na wenye sifa za ziada kufanya kazi kwenye halmashauri zote nchini.

Maelekezo hayo ameyatoa wakati wa majumuisho ya ziara ya kamati ya Bunge ya LAAC yaliyofanyika katika halmashauri ya Mji Kondoa mkoani Dodoma.

Aidha Mdee amesema Ofisi ya Rais TAMISEMI ifuatilie na kuchukua hatua kwa aliyehusika na ukiukwaji wa miongozo ya ujenzi wa shule ya KeiKei na kutumia michoro tofauti ya na ile iliyotolewa na ofisi ya Rais - TAMISEMI.

Pia amemtaka mkurugenzi wa halmashauri ya Mji wa Kondoa kuhakikisha taarifa za gharama halisi za utekelezaji wa mradi wa shule ya sekondari Keikei zinapatikana na kuwasilishwa kwa CAG kwaajili ya uhakiki.

‘Kondoa DC ilikuwa na miradi mitatu ambayo ni jengo la utawala, hospitali na shule ambayo yote inaonekana haukua madhubuti” Mdee

“Kutokana na ubadhilifu wa fedha uliobainika katika mradi wa shule ya sekondari Tura Ofisi ya Rais TAMISEMI ichukuwe hatua stahiki kwa watendaji wote walio husika katika kukwamisha utekelezaji wa mradi huu” amesema Mdee

Naibu katibu mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa anayeshughulikia Elimu Dkt. Charles Msonde ametoa maelekezo kwa niaba ya waziri wa nchi Ofisi ya Rais – TAMISEMI kwa makatibu tawala wa mikoa wote nchini kuhakikisha wanakua na ufuatiliaji wa karibu katika utekelezaji wa miradi yote ambayo inapata fedha kutoka Serikali Kuu.

Share: