Kutokuhudhuria mahakamani kumemponza, Kanye West afungiwa kampuni zake zote

Kanye West ameendelea kukutana na changamoto za kisheria kuhusiana na shule yake binafsi ya Donda Academy. Kwenye kikao cha mahakama kilichofanyika Desemba 13, 2024, Kanye West alishindwa kufika, na kusababisha Jaji Christopher K. Lui kutoa hukumu ya kifungo kwa kampuni tatu za Kanye, ambazo ni Yeezy Christian Academy, Donda Services LLC, na Stokes Canyon LLC.

Mashitaka haya yanatokana na kesi ya kuvunjwa kwa mkataba iliyowasilishwa na Isaiah Meadows, aliyekuwa mfanyakazi wa Donda Academy. Meadows anadai kwamba alikumbana na hali mbaya katika shule hiyo, ikiwa ni pamoja na mfumo wa usafi mbaya, nyaya za umeme zilizokuwa wazi, na madirisha yaliyokosa vioo, kwa sababu ya mapenzi ya ubunifu wa Kanye.

Hali ya kisheria ya Kanye West inazidi kuwa ngumu, hasa baada ya kuachana na wakili wake, Brian Brumfield, aliyejiondoa kutokana na kutokuwepo na maelewano kati yao. Hakimu Lui amesisitiza kuwa kesi hiyo itaendelea bila kuchelewa, na Kanye sasa atahitaji kujitetea mwenyewe kwenye kesi hiyo, ambayo inatarajiwa kuendelea mwaka ujao.

Mashitaka haya ni sehemu ya muendelezo wa changamoto za kisheria dhidi ya Ye na kampuni zake, hasa baada ya kauli zake za kibaguzi za mwaka 2022 ambazo zilisababisha kuvunjika kwa mikataba yake na makampuni makubwa kama Adidas na Gap.

Share: