Kupambana na ugaidi hakumaanishi kuibomoa gaza - macron

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amesema kupambana na "ugaidi" hakumaanishi "kuibomoa Gaza au kushambulia raia bila kujali".

Akizungumza na shirika la utangazaji la France 5, alitoa wito kwa Israel kukomesha mbinu zake za sasa za kivita "kwa sababu hazifai, kwa sababu maisha ya kila mtu yana thamani sawa na ya wale tunaotetea".

Kwa mujibu wa shirika la habari la AFP, Macron pia aliunga mkono "haki ya Israel ya kujilinda na kupambana na ugaidi", na kutoa wito wa kulindwa kwa raia na "maafikiano ya kusitisha mapigano kwa maslahi ya kibinadamu".

Share: