Korea kaskazini yarusha kombora aina ya hwasong-18

Shirika la habari la serikali KCNA limeripoti kuwa kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un alihudhuria hafla ya urushaji wa kombora hilo.

Kombora hilo la Hwasong - 18 lilifika umbali wa kilomita 6,518 sawa na maili 4,050 na kulenga shabaha iliyokusudiwa.

Kim Jong Un amesema kurushwa kwa kombora hilo kunatuma "ishara wazi kwa maadui ambao wanaendeleza uhasama" dhidi ya Korea Kaskazini.

Kiongozi huyo amefafanua kuwa hio ni mojawapo ya hatua ambayo Korea Kaskazini inaweza kuchukua iwapo Marekani itafanya uamuzi mbaya dhidi yake.

Share: