Koffi olomidé atangaza nia ya kuwania kiti cha seneti nchini drc

Antoine Christophe Agbepa Mumba, maarufu Koffi Olomidé, ametangaza nia ya kuwania kiti cha Seneti nchini DRC.

Nguli huyo wa muziki kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo atagombea Jimbo la Sud-Ubangi, lililo kaskazini-magharibi mwa nchi hiyo kupitia chama cha AFDC-A, katika uchaguzi utakaofanyika April 22.

 “Unaponisikiliza nikizungumza, inaokena dhahiri: naipenda nchi yangu. Naipenda Kongo na napenda ustawi wa watu wa Kongo. Naumia sana ninapoona watu wakiwa katika raha na furaha wakitumia mabilioni ya fedha huku wengine wakikosa milo kwa siku mbili, tatu hadi nne”, alisema Olomide.

Share: