Kim jong un atembelea viwanda vya uzalishaji silaha

Shirika la habari la serikali ya Korea Kaskazini KCNA limeripoti siku ya Jumatano kuwa Kiongozi wa nchi hiyo Kim Jong Un alitembelea wiki hii viwanda vya uzalishaji silaha.

Katika ziara hiyo, Kim alikosoa kile alichokiita "mapungufu" katika mfumo wa utengenezaji wa baadhi ya silaha huku akitoa wito wa kufanyika marekebisho na kusisitiza "umuhimu wa kimkakati wa uzalishaji wa silaha kubwa.

Kim Jong Un amegusia pia mahusiano mabaya na jirani yake Korea Kusini na kuishutumu Seoul kuchochea mapigano huku akihimiza nchi yake kuimarisha nguvu zake za kijeshi pamoja na kuzidisha uwezo wa kujilinda wa silaha zake za nyuklia.

Share: