Kwa mujibu wa KNCA, Kim amewasilisha mbele ya wajumbe ripoti pana ya tathmini ya uchumi wa taifa ambao amesema unastawi vizuri chini ya misingi ya kikomunisti.
Kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Yong Un, amesema mwaka 2023 umekuwa wa mabadiliko makubwa kwenye taifa hilo, akisifu mafanikio yaliyopatikana ndani ya jeshi na sekta nyingine ikiwemo uchumi, sayansi na afya ya umma.
Hayo yameripotiwa na shirika la habari la Korea Kaskazini, KNCA, likinukuu matamshi ya Kim wakati wa hotuba yake ya kuufungua mkutano wa kila mwaka wa Kamati Kuu ya chama tawala cha kikomunisti cha nchi hiyo.
Kwa mujibu wa KNCA, Kim amewasilisha mbele ya wajumbe ripoti pana ya tathmini ya uchumi wa taifa ambao amesema unastawi vizuri chini ya misingi ya kikomunisti.
Mkutano huo unafanyika siku chache kabla ya kumalizika mwaka 2023 ambao umeshuhudia Korea Kaskazini ikijitangaza rasmi ndani ya katiba yake kuwa dola yenye uwezo wa nyuklia na kufanikiwa kurusha satelaiti ya kwanza ya kijeshi miezi michache iliyopita.