Waziri wa Fedha Dkt Mwigilu Nchemba amesema Dola sio fedha ya Tanzania na hakuna mamlaka yeyote inayochapisha dola hapa Tanzania hivyo kupata dola inategemea na shughuli za uzalishaji zinazofanyika nchini ambapo katika matumizi ya dola moja ni kulipa deni la taifa ambalo hulipwa kwa dola na baadhi ya mikataba husainiwa kwa dola.
Amesema sekta ya Kilimo ni miongoni mwa sekta zinazotuwezesha kupata dola nchini, hivyo uzalishaji wowote katika sekta ya kilimo unaotusaidia kupunguza matumizi ya dola kwa kutoagiza bidhaa za nje serikali itaendelea kuwezesha uzalishaji huo ili kusaidia Kukabiliana na tatizo la matumizi ya dola kwa kuagiza bidhaa kutoka nje ambapo pia ametoa wito kwa wawezekaji kuendelea kulipa kodi na wafanyabiashara kuto kukwepa kodi na vitendo vyovyote vya kutolipa kodi kwa wakati.