Kenya yaanza kuondoa vikosi vya kijeshi Nchini dr congo

Kikosi cha kanda ya Afrika Mashariki kimeanza kuondoka katika eneo lenye matatizo la mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Wanajeshi hao walitumwa kwa mara ya kwanza katika eneo hilo mwezi Novemba mwaka jana kutokana na ombi la serikali ya Kongo kwa matumaini ya kulidhibiti kundi la waasi la M23 lililofufuka tena.

Lakini Kinshasa tangu wakati huo imekosoa jeshi la Afrika Mashariki kuwa halifanyi kazi, na imekataa kurejesha mamlaka yake.

Vikosi viwili vya wanajeshi wapatao 100 wa Kenya waliruka nje ya uwanja wa ndege wa Goma, mji mkuu wa jimbo la Kivu Kaskazini, mapema Jumapili.

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo inatazamiwa kufanya uchaguzi mkuu tarehe 20 Disemba.

Share: