Uamuzi huo pia umechangiwa na kauli ya Mkurugenzi wa Tume ya Maadili na Kupambana na Rushwa (EACC) Twalib Mbarak aliyetoa ushahidi kuwa mmoja kati ya Maafisa wa tume hiyo alinusurika kupigwa risasi na Askari hao wakati akitekeleza majukumu yake.
Zuio hilo limewekwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) Japhet Koome baaada ya kuwepo kwa ongezeko la Malalamiko ya Wananchi kuwa baadhi ya Askari wa Barabarani wamekuwa wakitumia vibaya silaha zao ikiwemo kushambulia raia hata wasioweza kusababisha madhara.
Uamuzi huo pia umechangiwa na kauli ya Mkurugenzi wa Tume ya Maadili na Kupambana na Rushwa (EACC) Twalib Mbarak aliyetoa ushahidi kuwa mmoja kati ya Maafisa wa tume hiyo alinusurika kupigwa risasi na Askari hao wakati akitekeleza majukumu yake.
Ripoti mbalimbali kutoka Mataifa mengi ya Afrika zimekuwa zikionesha Maafisa wa Usalama wakiwemo Askari Polisi wamekuwa wakitumia Silaha zao kinyume na Sheria ikiwemo kujeruhi na kuua Raia kwa kisingizio cha masuala ya Usalama au Kujilinda.