Kenya kusitisha utoaji wa viza kuanza januari

Rais wa Kenya William Ruto Jumanne alitangaza kuwa serikali yake imeamua kukomesha mahitaji ya viza kwa wageni wote duniani kuanzia Januari 2024.

Hayo aliyasema wakati wa sherehe za miaka 60 ya Jamhuri katika bustani ya Uhuru Gardens, Nairobi, ambapo alibainisha kuwa ukomeshaji huo unatokana na msingi wa kukumbatia utandawazi na kufungua mipaka ili kuchochea maendeleo ya kijamii na kiuchumi nchini.


"Kuanzia Januari 2024, Kenya itakuwa nchi isiyo na visa. Haitahitajika tena kwa mtu yeyote kutoka kona yoyote ya dunia kubeba mzigo wa kutuma maombi ya visa ili kuja Kenya," alisema Ruto.

Share: