Kenya: kambi ya kijeshi ya uingereza batuk wanajeshi wake walalamikiwa kutelekeza watoto

Serikali ya Uingereza inailipa Kenya takriban Tsh. Bilioni 1 kila Mwaka kwaajili ya kibali cha kuruhusu Wanajeshi wake

Baadhi ya Wanawake wanaoishi karibu na Kambi ya Mafunzo ya Kijeshi inayoongozwa na Jeshi la Uingereza ya BATUK wamelalamikia kutelekezwa na Wanajeshi wanaotuhumiwa kuwabaka na kuwaachia Watoto bila msaada wowote

Ripoti ya CNN imeeleza mamia ya Wanawake wameandika malalamiko hayo kwenda kwa Serikali ya Uingereza na Jeshi la nchi hiyo wakitaka kujua hatma juu ya Haki zao tangu Mwaka 2011

Pia, imeelezwa tayari Kamati ya Bunge ya Ulinzi na Uhusiano wa Mambo ya Nje inaendelea na uchunguzi kuhusu tuhuma zilizotolewa na Wananchi juu ya Kambi hiyo na itaanza kuwasikiliza Maafisa wake mwisho wa Mwezi Juni 2024

Aidha, ripoti inaonesha Serikali ya Uingereza inailipa Kenya takriban Tsh. Bilioni 1 kila Mwaka kwaajili ya kibali cha kuruhusu Wanajeshi wake kuweka kambi kufanya mazoezi Nchini humo. 

Share: