Moja wapo ni Watoto waliozaliwa na Maambukizi ambao sasa wamekuwa vijana au Watu wazima kujihusisha na Ngono bila kuchukua tahadhari.
Kwa mujibu wa taarifa ya Chuo Kikuu cha Hospitali ya Aga Khan cha jijini Nairobi, sababu mbili zimebainika kuwa chanzo cha ongezeko hilo na Moja wapo ni Watoto waliozaliwa na Maambukizi ambao sasa wamekuwa vijana au Watu wazima kujihusisha na Ngono bila kuchukua tahadhari.
Dkt. Adeel Shah, Bingwa wa Magonjwa ya Kuambukiza na Watoto kutoka Aga Khan amesema "Vijana hawa na Watu Wazima wamekuwa Kundi la Maambukizi, wanaingia kwenye mahusiano na wenzao wasio na VVU na kushiriki ngono bila kinga, hali inayowaweka watu wengi zaidi katika maambukizi".
Sababu nyingine ni Vijana waliogeuza miili yao kama Kitega Uchumi kwa kujihusisha na Ngono na watu wazima kwa lengo la kujipatia Fedha, matokeo yake wengi wameishia kupata Maambukizi ya VVU na Magonjwa mengine ya Zinaa kwasababu wengi wanaokutana nao wanawapa masharti ya kutotumia Kinga.
Riipoti ya mpya ya Maambukizi ya Virusi Vya UKIMWI Nchini Kenya, imeonesha ongezeko la Watu 32,017 huku Vijana wakiwa 11,229 na wengi wao ni wenye umri wa miaka kati ya 15 hadi 24.