Keir starmer ateuliwa kuwa waziri mkuu wa uingereza baada ya kumzidi kwa kura rishi sunak

Vyama vingine vilivyohusika kwenye uchaguzi huo ni pamoja na Reform UK, Liberal Democrats, Democratic Unionist Party, Green

WAZIRI Mkuu mteule wa Uingereza Keir Starmer ameahidi kuanza “enzi mpya ya kitaifa" baada ya Chama chake cha Labour kumaliza utawala wa Conservative uliodumu kwa miaka 14.

Baada ya uchaguzi wa jana Julai 4, 2024, Starmer kutoka Chama cha Labor aliibuka kidedea na kumbwaga aliyekuwa Waziri Mkuu Rishi Sunak wa Conservative.

Vyama vingine vilivyohusika kwenye uchaguzi huo ni pamoja na Reform UK, Liberal Democrats, Democratic Unionist Party, Green, Scottish National Party (SNP) na Plaid Cymru na vinginevyo.

Starmer anakabiliwa na changamoto ya kushughulikia masuala mbalimbali yakiwemo ukuaji wa uchumi, afya, uhalifu, ulinzi na usalama, makazi na Uingereza kujitoa Umoja wa Ulaya (Brexit).

Share: