KANYE WEST APIGWA MARUFUKU KUINGIA AUSTRALIA

Msanii maarufu wa Marekani Kanye West, ambaye kwa sasa anatumia jina la Ye, amepigwa marufuku rasmi kuingia nchini Australia baada ya serikali ya nchi hiyo kufuta visa yake ya utalii kutokana na wimbo wake unaodaiwa kuwa na ujumbe wa chuki dhidi ya Wayahudi na kumtaja Adolf Hitler.


Uamuzi huo mzito unamaanisha Ye hataruhusiwa kuingia nchini humo hata akiwa na mkewe mzaliwa wa Australia, Bianca Censori, ambaye alikulia katika jiji la Melbourne.


Inaelezwa kuwa Ye alikua tayari amepata visa ya utalii ambayo ingeweza kuwa halali kwa hadi mwaka mmoja, lakini serikali imeamua kuifuta rasmi kufuatia maudhui ya wimbo wake mpya, unaodaiwa kueneza kauli za chuki dhidi ya Wayahudi — jambo ambalo limezua hasira kubwa kimataifa.

Tufatilie kupitia kisumbuzi @startimestz CH 161 (antena) CH 401 (Dish) pamoja na kwenye YouTube channel yetu ya #STBongoTV Kwa Taarifa zaidi.


#STBongoUpdates #NyumbaniKwanza


Kwa hatua hii, Ye hawezi kuingia Australia kwa ziara yoyote rasmi au binafsi, labda mpaka serikali ya nchi hiyo iamue kubadili msimamo wake


Tufatilie kupitia kisumbuzi @startimestz CH 161 (antena) CH 401 (Dish) pamoja na kwenye YouTube channel yetu ya #STBongoTV Kwa Taarifa zaidi.


#STBongoUpdates #NyumbaniKwanza


Share: