Kamati ya baraza la wawakilishi yazuru ofisi za kumbukumbu na nyaraka dsm.

Kamati ya Kusimamia Ofisi za Viongozi wa Kimataifa ya Baraza la Wawakilishi ikiongozwa na Mwenyekiti Wake Bwana Machano Othumani Machano na Waziri wa Nchi ya Rais Zanzibar Bwana Jamal Kassim wametembelea Ofisi za Hifadhi ya Nyaraka na Kumbukumbu Tanzania Bara katika mji wa Dar Es Salaam na kulakiwa na mwenyeji wao Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi na Utawala Bora Ndg. Ridhiwani Kikwete.

Mwenyekiti wa kamati Bwana Machano, ameshukuru Ofisi ya Rais kwa kuwakarobisha na kuwapa nafasi ya kujifunza. Ni fursa nzuri kwa kamati lakini kwa serikali pia kwa kuwapa nafasi ya kujua jinsi ya uhifadhi wa kumbukumbu na kwamba wameona jinsi ya kutunza historia ya nchi. Pia wameomba kuimarishwa kwa mahusiano baina ya pande hizi mbili.

Akizungumza Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ndg. Jamal Kassim, ameomba kuimarisha mahusiano baina ya ofisi hizi mbili ili kuleta tija na hasa akisisitiza katika kuhakikisha kumbukumbu za wahasisi haswa Hayati Sheikh Abeid Amani Karume zinawekwa vizuri sana kwa faid ya Taifa na vizazi vijavyo.

Akizungumza baada ya kuwapokea, Naibu Waziri Ndg. Kikwete ameupongeza uongozi wa serikali ya Mapinduzi kwa kutoa kipaumbele kwa uhifadhi wa Nyaraka na kumbukumbu kwa kutenga bajeti na uamuzi mkubwa wa kuzihifadhi ili kusaidia nchi inajua imetoka wapi na inakwenda wapi! Ni jambo zuri sana. Pia amewahakikisha kamati na serikali ya Zanzibar utayari wa Serikali na ofisi ya Rais kushirikiana kuhakikisha kuwa msaada wowote kusaidia kuimarisha ofisi ya Nyaraka na kumbukumbu .

Share: