Judith tuluka anakuwa wa mwanamke wa kwanza kwenye historia ya drc congo kushikilia nafasi ya waziri mkuu.

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Felix Tshisekedi, amemteua Waziri wa Mipango, Judith Tuluka Suminwa kuwa waziri mkuu mpya wa nchi hiyo.

Hii ni mara ya kwanza katika historia ya DRC ambapo mwanamke atashikilia nafasi ya waziri mkuu.

Msemaji wa Tshisekedi alisema kwenye televisheni ya taifa siku ya Jumatatu kwamba uteuzi wa Suminwa unaanza kutekelezwa mara moja.

"Najua kwamba kazi ni kubwa na changamoto ni kubwa, lakini kwa msaada wa rais na wa kila mtu, tutafika," Suminwa alisema kwenye mkutano na waandishi wa habari siku ya Jumatatu baada ya uteuzi wake.

Share: