Jet: serikali imeshauriwa kuingiza somo la mazingira katika mitaala ya elimu kuanzia ngazi ya chini

Elimu tunayofundishwa Shule ni kufagia, kupanda na kumwagilia maua, hiyo ni sehemu ndogo sana.

Serikali imeshauriwa kuingiza Somo la Mazingira katika Mitaala ya Elimu kuanzia ngazi ya chini na liwe endelevu ili kuifanya jamii kubadilika na kusaidia kukabiliana na changamoto za uharibifu wa Mazingira unaosababisha Mabadiliko ya Hali ya Hewa

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Chama cha Waandishi wa Habari za Mazingira Tanzania (JET), Ellen Utaru Okoedion amesema hayo na kuongeza “Elimu tunayofundishwa Shule ni kufagia, kupanda na kumwagilia maua, hiyo ni sehemu ndogo sana. Kuna uharibifu mwingi wa mazingira unafanyika kwa kujua au kutojua na hiyo inachangia Mabadiliko ya Hali ya Hewa na madhara mengine.”

Aidha, amedai uzoefu unaonesha Watu wanaokua katika mazingira mazuri mara nyingi wanakuwa na fikra chanya pia katika maisha yao ya kila siku


Share: