Jeshi la polisi limetoa wito kwa viongozi wa nyumba za ibada kipindi hiki cha sherehe za ijumaa kuu na pasaka

Jeshi la polisi nchini Tanzania limetoa wito kwa kwa viongozi wa nyumba za ibada ambao watakuwa na ibada katika kipindi hiki cha Juma kuu wawasiliane na viongozi wa polisi katika maeneo yao ili washirikiane katika kuimarisha usalama kipindi cha sikukuu za Pasaka.

David Misime Msemaji wa jeshi la polisi nchini Tanzania ametoa wito pia kwa wananchi wote kuendelea kuzingatia kanuni za kiusalama inayosema usalama unaanza na mimi mwenyewe.

Aidha polisi pia imesema inaendelea kujiimariaha vizuri ili kuhakilisha kwamba ibada na sherehe hizo zinafanyika katika hali ya amani, utulivu na usalama wa kutosha kwa kufanya doria katika mitaa na barabara zote kuu ili kuzuia uhalifu au uvunjifu wowote ule wa amani.

Tarehe 31 machi waumini wa dini ya kikristo wataungana na wenzao duniani katika kusherehekea sikukuu ya pasaka, sherehe ambazo hutanguliwa na mikusanyiko na ibada mbalimbali ambazo hufanyika nyakati za mchana na usiku kwa siku za alhamisi, Ijumaa, jumamosi na jumapili ya pasaka.

Share: