JESHI LA ISRAEL LASHAMBULIA 'MAENEO' 150 YA GAZA KWA MABOMU NA KUFUNGUA "NJIA YA MUDA " KWA WAKAZI KUONDOKA

Jeshi la Israel limesema Jumatano kuwa limepiga "maeneo zaidi ya 150" katika mji wa Gaza tangu kupanua mashambulizi yake ya ardhini Jumatatu jioni.

"Katika muda wa siku mbili zilizopita, jeshi la anga na mizinga imeshambulia zaidi ya shabaha 150 za magaidi katika eneo lote la Gaza ili kuunga mkono vikosi vya kudhibiti katika eneo hilo," taarifa ya jeshi imesema.


Hapo awali, jeshi lilitangaza kuanzishwa kwa "njia ya muda ya kupita" kwa wakazi wa mji wa Gaza kutoroka, kufuatia upanuzi wa mashambulizi ya ardhini na mashambulizi ya mabomu katika miji mikubwa ya Ukanda huo.

Msemaji wa jeshi Avichay Adraee alichapisha taarifa kwenye jukwaa la X, akisema, "Ili kuwezesha harakati za kusini, njia ya muda imefunguliwa kupitia Mtaa wa Salah al-Din," akibainisha kuwa harakati za kupita kwenye njia hizi zitakua "kwa saa 48," kuanzia Jumatano alasiri na kumalizika Ijumaa alasiri.

Shirika la utangazaji la Israel liliripoti kuwa kitengo cha 36 kinatarajiwa kujiunga na operesheni ya kijeshi katika siku zijazo, na kuongeza kuwa jeshi linakadiria kuwa operesheni hiyo inaweza kudumu kati ya "miezi miwili hadi mitatu."

Share: