Katika taarifa mpya, Jeshi la Ulinzi la Israel linasema kuwa wanajeshi wake wamefanikiwa kudhibiti kile inachokiita "robo ya sehemu" ya mji mkubwa wa Gaza - karibu na uwanja wa Palestina katika eneo la al-Rimal.
Jeshi la Israel linasema kuwa limepata mtandao wa handaki uliowahi kutumiwa na uongozi wa juu wa Hamas katika mji wa Gaza, ambao unauelezea kama "mji wa kigaidi wa chinichini".
Katika taarifa mpya, Jeshi la Ulinzi la Israel linasema kuwa wanajeshi wake wamefanikiwa kudhibiti kile inachokiita "robo ya sehemu" ya mji mkubwa wa Gaza - karibu na uwanja wa Palestina katika eneo la al-Rimal.
IDF inasema baada ya wiki kadhaa za mapigano majeshi yake yalichukua udhibiti wa eneo katika mji mkubwa zaidi wa Gaza, ambayo inasema ndipo "uongozi wa utawala wa kijeshi wa Hamas ulifanya kazi" - ikiwa ni pamoja na viongozi wa kisiasa kama Ismail Haniyeh, na makamanda wa kijeshi Yahya Sinwar na Muhammad Deif.
Inaongeza kuwa Palestine Square ni kitovu cha "mtandao wa handaki wa kimkakati", unaounganisha na "miundombinu ya chini ya ardhi katika eneo la Hospitali ya Rantisi na Hospitali ya Shifa".
DF ilishiriki picha za video za wanajeshi wakichunguza msururu wa vichuguu na picha za satelaiti na milango inayodaiwa kuwekewa alama, lakini hakuna ushahidi wowote unaoonesha kuunganishwa na hospitali yoyote uliyotajwa.
Pia inasema mihimili ambayo ni sehemu ya "mji wa kigaidi wa chinichini" ilijengwa katika "makazi na ofisi za maafisa wakuu", ambayo ilitumika kuelekeza "shughuli za uendeshaji" za Hamas na "harakati za kila siku zinazolindwa kupitia katikati ya jiji la Gaza".