Jay Z akanusha kumbaka binti wa miaka 13 akiwa na P Didy
Baada ya Rapper Jay Z kutajwa kwenye tuhuma za kuhusika kwenye tukio la kumbaka binti wa miaka 13 mnamo mwaka 2000 akiwa pamoja na P'Diddy, nguli huyo wa rap kupitia mwanasheria wake amekanusha vikali tuhuma na taarifa hizo.
Jigger kupitia mwanasheria wake amedai kuwa tuhuma hizo zinalenga kumuharibia taswira yake katika jamii na kujenga picha mbaya kwa watoto wa kike, huku akitajakesi hiyo imesukwa kwa lengo la kutaka kupata pesa kutoka kwake kwa sababu ya faida zao binafsi.
Share: