Jasusi wa zamani wa israel zvi zamir (98) afariki dunia

Zamir, ambaye aliongoza shirika hilo kati ya 1968 na 1974, alianzisha mkakati ambao bado unadumu wa watendaji wa siri nje ya taifa lake katika kuwaangamiza maadui wa Israeli.

Aliyekuwa mkuu shirika la ujasusi la Israel, Mossad, Zvi Zamir, ambaye aliongoza shirika hilo wakati wa vita vya Waarabu na Israel vya 1973, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 98.

Zamir, ambaye aliongoza shirika hilo kati ya 1968 na 1974, alianzisha mkakati ambao bado unadumu wa watendaji wa siri nje ya taifa lake katika kuwaangamiza maadui wa Israeli. Taarifa ya serikali ya Israel imesema kwamba Zamir amefariki dunia nchini humo Jumatatu usiku. Mossad iliongoza oparesheni kabambe za kukabiliana na ugaidi chini ya uongozi wake, ikiwa ni pamoja na juhudi za kimataifa za kuwaondoa viongozi wa kundi la wanamgambo wa Palestina Black September, ambalo lililaumiwa kwa mauaji ya mwaka 1972 ya wanariadha wa Olimpiki wa Israel huko Munich, Ujerumani.

Share: