Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki January Makamba amesema taarifa iliyoripotiwa na baadhi ya Vyombo vya Habari Nchini ikidai kuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) imetambulisha noti mpya itakayotumika katika Nchi Wanachama iitwayo SHEAFRA, sio taarifa yenye ukweli.
Kupitia ukurasa wake wa X, Makamba amesema “Hizi taarifa si za kweli, taaarifa na vigezo vya kiuchumi na kitaasisi vya kufikiwa kwa Umoja wa Fedha (Monetary Union)/Sarafu Moja (Single Currency) kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki bado kukamilika, mapendekezo ni kufika hatua hiyo mwaka 2031.”
Inaaminika Vyombo vingi vya Habari viliandika habari hiyo baada ya kuiona kwenye akaunti ya X iitwayo Government of East Afrika ambayo sio akaunti rasmi ya Jumuiya.
Share: