Israel yagundua handaki kubwa zaidi linalotumiwa na hamas

Jeshi hilo la IDF limeongeza kuwa, handaki hilo limegunduliwa karibu mita 100 kusini mwa kituo cha ukaguzi cha Erez, ambacho ni kivuko cha mpaka kati ya Israel na Gaza.

IDF imelitaja handaki hilo kama moja ya nyenzo muhimu za kundi la Hamas ambalo hutumiwa kupitisha vifaa na bidhaa nyengine za wapiganaji wa Hamas kutoka Gaza hadi kwenye mpaka wa Israel.

Msemaji mkuu wa jeshi la Israel Rear Admiral Daniel Hagari amesema hilo ni handaki kubwa zaidi kuwahi kuliona huko Gaza na kwamba fedha na muda mwingi ulitumika kulijenga handaki hilo.

Jeshi hilo pia limeeleza kuwa, limepata silaha nyingi zilizokuwa zimehifadhiwa kwenye handaki hilo, tayari kutumika kufanya mashambulizi.

Share: