Israel itakuwa na 'jukumu la usalama kwa ujumla' kwa gaza - netanyahu

Israel itakuwa na "jukumu la jumla la usalama" kwa Ukanda wa Gaza kwa "muda usiojulikana" mara tu mapigano yatakapomalizika, waziri mkuu wa nchi hiyo amesema.

Israel itakuwa na "jukumu la jumla la usalama" kwa Ukanda wa Gaza kwa "muda usiojulikana" mara tu mapigano yatakapomalizika, waziri mkuu wa nchi hiyo amesema.

Benjamin Netanyahu alitoa maoni hayo katika mahojiano na kituo cha Marekani cha ABC News, ambapo pia alitupilia mbali wito wa kusitishwa kwa mapigano bila ya kuachiliwa kwa mateka waliochukuliwa na Hamas katika mashambulizi yao ya Oktoba 7.

Hata hivyo, alisema kusitishwa kwa misaada ya kibinadamu huenda kukawezekana.

"Kuhusu kusitishwa kwa vita kidogo kimkakati - saa moja hapa, saa moja pale - tumekuwa nayo awali. Nadhani tutaangalia mazingira, ili kuwezesha bidhaa na misaada ya kibinadamu kuingia, au mateka wetu na mateka wa kibinafsi kuondoka," alisema.

Share: