nguvu ya kuaminika itahitajika kuingia katika eneo hilo ikiwa ni lazima ili kuzuia kuibuka kwa vitisho vya wanamgambo
Waziri mkuu wa Israel anasema nchi hiyo haitaki kuliteka, kukalia au kutawala Ukanda wa Gaza baada ya vita vyake na Hamas kumalizika.
Benjamin Netanyahu alikiambia kituo cha televisheni cha Marekani Fox News kwamba "nguvu ya kuaminika" itahitajika kuingia katika eneo hilo ikiwa ni lazima ili kuzuia kuibuka kwa vitisho vya wanamgambo.
"Hatulengi kuteka Gaza, hatutaki kuikalia Gaza, na hatutaki kuitawala Gaza," alisema, akiongeza kuwa serikali ya kiraia itahitajika, lakini Israeli pia itahitaji hakikisho kwamba shambulio kama lile la Oktoba 7, ambalo Hamas liliua watu wapatao 1,400, halitokei tena.
"Kwa hiyo, tunapaswa kuwa na kikosi cha kuaminika ambacho, ikibidi, kitaingia Gaza na kuwaua wauaji. Kwa sababu hilo ndilo litakalozuia kuibuka tena kwa kundi linalofanana na Hamas," alisema.
Maoni ya Netanyahu mapema wiki hii yalikuwa yamependekeza kuwa Israeli itawajibika kiusalama usalama huko Gaza, na kutoa majibu makali kutoka kwa Marekani