Ilala wahimizwa kuhusu chanjo za watoto

Wizara ya Afya imekusudia kutoa chanjo kwa watoto zaidi 2000 ambao hawakupata chanjo na watoto 1700 ambao hawakumalizia chanjo huku wito ukitolewa kwa jamii kutoa ushirikiano watoto kupatiwa chanjo ili kuimarisha kinga ya mwili dhidi ya Magonjwa yanayozuilika kwa chanjo.

Akizindua rasmi Mfumo wa uraghibishaji wa Huduma za Chanjo Wilaya ya Ilala, Dar es Jijini Salaam, Mkuu wa wilaya hiyo, Edward Mpogolo, amesema watoto 2550 hawakupata chanjo kutokana na sababu mbalimbali na watoto 1753 pia hawakumalizia chanjo zao wilayani humo .

Amesema kwa kutumia afua ya uraghibishaji wa Chanjo kwa Viongozi wa Kijamii kupitia Programu ya "Human Centred design,HCD inayowezeshwa na UNICEF kwa kutasaidia makundi hayo mawili itakuwa rahisi kupata huduma kupitia mfumo huo kwa urahisi huku akiwapongeza Wataalam kutoka Wizara ya Afya, Sehemu ya Elimu ya Afya kwa Umma, Ofisi ya Rais TAMISEMI, pamoja na Jiji la Dar Es Salaam kwa kuja na Programu hiyo.

Aidha, Mpogolo amesema ni muhimu kila mmoja kuweka mikakati kabambe katika kuhakikisha kila kila mtoto aliye na umri chini ya miaka 5 kupata chanjo katika kumkinga dhidi ya magonjwa mbalimbali.

Afisa Program ya Uratibu na Elimu ya Afya Maeneo ya Kazi kutoka Wizara ya Afya, Sehemu ya Elimu ya Afya kwa Umma, Simon Zilimbili, amesema chanjo hiyo itaendeshwa kwa siku 10 katika tarafa mbili(Ukonga na Segerea) kati ya tatu za Wilaya ya Ilala ambapo kupitia mpango huo utasaidia kuhakikisha kila mtoto anapata chanjo.

Kwa Upande wake Mratibu wa Chanjo Halmashauri Jiji la Dar Es Salaam Martine Kalongolela amesema lengo la zoezi hilo ni kufikia asilimia 100 huku akitoa hofu wananchi na zoezi na hali hiyo itasaidia kumkinga mtoto huku akitolea mfano madhara ya mtoto akikosa chanjo ya Polio ni kusababisha ulemavu au kifo.

Share: