Idadi ya wahitimu wa kiume yapungua chuo kikuu cha makerere uganda.

"Nimegundua , wahitimu wa kike ni zaidi ya wenzao wa kiume kwa asilimia 54. Chuo kinahitaji kuangalia upungufu huu wa idadi ya wahitimu wa kiume"

Kumekua na upungufu wa idadi ya wanafunzi wa kiume wanaohitimu chuo kikuu cha makerere katika mahafali ya hivi karibuni ikilinganishwa na wenzao wa kike. kati ya jumla ya wanafunzi 12,913 waliohitimu katika mahafali ya 74 yanayoendelea wiki hii, 6816 ni wanawake na 6097 ni wanaume. katika mahafali ya 73 mwaka jana walihitimu wanafunzi 13,221 ambapo wanawake ni 6809 (asilimia 52) na wanaume ni 6412(asilimia 48).Kupungua huku kumemshangaza Waziri wa elimu na michezo wa Uganda Bi Janet Museveni, ambaye alihimiza chuo kikuu hicho kushughulikia suala hilo.

"Nimegundua , wahitimu wa kike ni zaidi ya wenzao wa kiume kwa asilimia 54. Chuo kinahitaji kuangalia upungufu huu wa idadi ya wahitimu wa kiume" Bi Museveni, ambaye pia ni mke wa rais, alibainisha katika hotuba iliyosomwa kwa ajili yake na waziri wa serikali wa elimu ya juu, Bw John Chrysestom Muyingo, katika siku ya kwanza ya sherehe za kuhitimu 74 za chuo kikuu jana.

Aliongeza "hali hii inapita katika viwango vyote vya elimu, kwa hivyo, kuna hitaji la utafiti kwa chuo kikuu" Wakati wa matokeo ya mtihani wa kumaliza elimu ya msingi (PLE) wa 2023 ,Bi Museveni alielezea mtindo huo haufai . Kwa mujibu wa Baraza la Taifa la Mitihani la Uganda, jumla ya wanafunzi 749,347 waliomaliza shule ya msingi mwaka jana 391,558 walikua wasichana na 357, 789 walikua wavulana.

Share: