Idadi ndogo ya wapiga kura wamejitokeza katika uchaguzi wa jumapili hong kong.

Chini ya sheria mpya za uchaguzi, idadi ya wawakilishi waliochaguliwa moja kwa moja kwa wilaya 18 za jiji hilo, imepunguzwa kutoka karibu wote, hadi 88, ikiwa ni asilimia 20 ya jumla ya viti 470.

Wapiga kura ama walikuwa na wasiwasi, au kususia uchaguzi, ambao baadhi ya watu wanaona kama kurudisha nyuma demokrasia ya jiji.

Idadi ya wapiga kura waliojitokeza siku ya Jumapili katika uchaguzi wa halmashauri za wilaya huko Hong Kong ilikuwa ndogo, ikiwa ni mara ya kwanza tangu mfumo wa uchaguzi ulipobadilishwa mwaka huu ili kurejesha utulivu na kuimarisha udhibiti baada ya maandamano makubwa yanayoipinga serikali na yanayounga mkono demokrasia mwaka 2019.

Wapiga kura ama walikuwa na wasiwasi, au kususia uchaguzi, ambao baadhi ya watu wanaona kama kurudisha nyuma demokrasia ya jiji. Kufikia jioni kwa saa za huko, idadi ya wapiga kura waliojitokeza ilikuwa asilimia 24, ikiwa ni chini sana kuliko wakati wa uchaguzi wa halmashauri za wilaya uliopita wa mwaka 2019 ambao ulishuhudia idadi kubwa ya wapiga kura waliojitokeza kwa asilimia 71, hadi wakati vituo vya kupigia kura vilipofungwa usiku.

Chini ya sheria mpya za uchaguzi, idadi ya wawakilishi waliochaguliwa moja kwa moja kwa wilaya 18 za jiji hilo, imepunguzwa kutoka karibu wote, hadi 88, ikiwa ni asilimia 20 ya jumla ya viti 470.

Viti vilivyobaki vinateuliwa na mtendaji mkuu wa Hong Kong, ambaye anachaguliwa na Beijing, au anachaguliwa na wawakilishi, ambao wanateuliwa na serikali.

Share: